UJERUMANI KUFUTA MACHOZI DHIDI YA SWEDEN LEO? NI BONGE LA MECHI - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

UJERUMANI KUFUTA MACHOZI DHIDI YA SWEDEN LEO? NI BONGE LA MECHI


Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mexico katika mchezo wa kwanza wa kundi F, Ujerumani wanarejea tena dimbani leo.

Timu hiyo itakuwa inaumana na Sweden kuanzia majira ya saa 3 kamili usiku, mchezo ambao wanapaswa kupata matokeo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu kuingia hatua inayofuata.


Katika msimamo wa kundi F, Ujerumani haina alama hata moja huku Sweden na Mexico wakiwa na alama 3 kila mmoja kufuatia ushindi wa mechi zao za kwanza.

Wakati huo Korea Kusini nayo imeungana na Ujerumani kwa kuwa na idadi ya alama 0 huku wote wakisubiri hatima ya michezo yao inayofuata.

No comments:

Post a Comment