TUNISIA YAKUMBANA NA KIPIGO CHA MBWA KOKO KUTOKA UBELGIJI, LUKAKU ATUPIA MBILI KAMBANI - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

TUNISIA YAKUMBANA NA KIPIGO CHA MBWA KOKO KUTOKA UBELGIJI, LUKAKU ATUPIA MBILI KAMBANI


Tunisia imepokea msiba mwingine katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kukumbana na kipigo cha mbwa koko cha mabao 5-2 kutoka kwa Ubelgiji.

Katika mchezo huo wa Kundi G uliopigwa Uwanja wa Spartak, Ubelgiji wamejipatia mabao yao kupitia kwa Romelu Lukaku aliyefunga mawili.

Mabao mengine ya Ubelgiji yamewekwa kimiani na Eden Hazard aliyefunga mawili pia moja likiwa la penati, pamoja na Michy Batshuayi katika dakika ya 90.

Mabao ya Tunisia yamewekwa kimiani na Dylan Bronn katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza na Khaziri dakika ya 90+3.

Msimamo wa kundi hilo unaonesha Ubelgiji ipo kileleni ikiwa na alama 6 kisha ikifuatiwa na England yenye 3 huku Panama na Tunisia zikiwa hazijapata alama yoyote.

No comments:

Post a Comment