Tukio Zima la Ufunguzi wa World Cup Hili Hapa - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 14 June 2018

Tukio Zima la Ufunguzi wa World Cup Hili Hapa

Hayawayi hayawi sasa yamekuwa. Ndio. Ni zile Sherehe za ufunguzi wa Kombe la dunia Kule nchini Urusi. Ni muda wa kusahau makeke yaliyofanyika zile fukwe za Copa capabana kwenye fainali za kombe la dunia kulee brazili mwaka 2014. Mashindano haya yatasafiri umbali wa kilometa 11, 545 yaani kutoka jiji la Rio de Janeiro mpaka jini la Moscow ambapo ni sawa na maili 7174.

Katika Sherehe hizi wanasarakasi wasiopungua mia tano watatoa burudani mubashara.

Bila shaka Waswahili hawakukosea kunena ya kwamba kazi na dawa, Ikumbukwe vyema 2014 Wanamuziki Pitbull na Jenifer Lopez walituimbuiza kule Brazil.

Mwaka huu ni zamu ya Robbie Williams pamoja na mwanamuzi chipukizi kutoka Urusi Aida Garrifulina watatoa burudani la kipekee. Sherehe hizi zitafanyika katika uwanja wa Moscow’s Luzhniki Stadium unaobeba zaiddi ya watazamaji 80,000.

wasanii wakubwa wengine watakotoa burudani ni kama vile, Pianist Denis Matsuev, nyota wa global opera stars Anna Netrebko, Yusif Eivazov, Ildar Abdrazakov, na Albina Shagimuratova hao ni moja ya wanamuziki mashughuri watakaotoa burudani kali.

Tunafahamu kwamba wimbo wa Live It Up ulioimbwa na Will Smith, Nicky Jam pamoja na Kosovar, na msanii kutoa Albania Era Istrefi.

Kwa kawaida wasanii waliopewa jukumu la kuimba wimbo rasmi wa kombe la dunia huwa wanatumbuiza.

Wimbo wa Colors uliteuliwa kuwa wimbo rasmi wa Cocacola kwenye matangazo yao yanayohusiana na kombe la dunia.

Tuitazamie mchezo wa ufunguzi. Katika mchezo wa ufunguzi Urusi watakutana na Saudia. Naam tufahamu kidogo kuhusu kikosi cha Urusi na historia yao.

Mchezo huo utachezwa saa 11 kamili nusu Saa mbele baada ya sherehe za ufunguzi kutia Nanga.
Warusi wamejipanga kwelikweli. Hawana utani. Walipopoleka ombi la kuandaa fainali hizi kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2008. Wakati ule walifika fainali la kombe la mataifa ya ulaya.

Maisha yamebadilika sana. Kwa sasa wapo nafasi ya 70 kwenye viwango vya FIFA. Na hii ni fainali zao za 11 tokea mwaka 1958. Kwenye kikosi chao mchezaji hatari ni fyodor Smolov mwenye mabao 12 katika michezo 32. Hata hivyo katika kikosi chao hakuna mchezaji mwenye magoli zaid ya 12. Mpaka Sada Urusi imefunga magoli 66 na kuruhusu magoli 47. Wameshinda michezo 17 na kupoteza 15 katika michezo 40 ya kombe la dunia.

Mwaka 1966 walimaliza nafasi ya 4 katika kombe la dunia. Kuanzia mwaka 1930 mpaka mwaka 1990 Urusi walishiriki kombe la dunia kupitia umoja wa nchi za kisoshalist kabla ya muungano huo wa soviet kuanguka.

Katika zile timu bora duniani Hatuwezi kuitaja Urusi. Haijawahi kufuzu hatua yoyote ya makundi tokea 2008. Katika michezo yake 7 ya mwisho hawajapata ushindi wowote. Mara yao ya mwisho kushinda ni mwaka 2017 mwezi wa 10. Kwa sasa

Tuitazamie timi ya taifa ya Saudia
Katika michezo 10 ya mwisho ya Saudia 10 wamefungwa michezo 6 na kushinda miwili na suluhu. Kwa sasa kwenye viwango vya FIFA wapo nafasi ya 67 mwaka 2004 walizalisha kizazi cha dhahabu ambacho kiliipandisha Haifa hill hali nafasi ya 20.

Katika Kombe la Dunia wameshiriki Mara tano pekee. Rekodi yao kubwa walifanikiwa kuvuka hatua ya makundi Mara moja tu nayo ni mwaka 1994. Katika historia ya kombe la dunia imeshinda magoli 9 nankuruhusu magoli 32 katika michezo yote 13 iliyowahi kucheza katika fainali za kombe la dunia. Mchezaji wao tegemezi ni Mohamed Al Sahlawi anayechezea klabu Al Nassr. Pia wanamtegemea sana winga wao Fahad Al Muwallad ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Levante kwa mkopo.Imeandaliwa na Privaldinho (Instagram)

No comments:

Post a Comment