TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMANNE - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 26 June 2018

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO JUMANNE


Paris St-Germain imewapatia Manchester United ombi la mkataba wa kubadilishana kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba ,24, kwa beki wa Itali Marco Verratti pamoja na fedha.. (Sun)

Mshambuliaji wa West Ham Manuel Lanzini, 25, anatarajiwa kukosa msimu wote ujao kutokana na jeraha la goti alilopata wakati wa mazoezi nchini Argentina kabla ya mechi ya kombe la Dunia. (Mirror)

Manchester United inaweza kumpatia raia wa Uingereza Luke Shaw, 22, kandarasi mpya kwa sababu klabu hiyo haiko tayari kulipa dau la £60m kumsajili beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27. (Manchester Evening News)

West Brom imekataa ombi la £12m kutoka kwa West ham ili kumnunua beki wa Uingereza Craig Dawson, huku klabu hiyo ikisema kuwa mchezaji huyo ana thamani ya £20m. (Telegraph)

Sevilla imesisitiza kuwa kiungo wa kati Ever Banega, 29, hauzwi msimu huu licha ya hamu kutoka kwa Arsenal (Independent)

Lyon inajiandaa kumpatia Nabil Fekir, 24, mkataba mpya ili kuizuia Liverpool kufufua matumaini ya kumsaka mshambuliaji huyo wa Ufaransa. (Mirror)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment