TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO IJUMAA - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 15 June 2018

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO IJUMAA


Arsenal wana nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Borussia Dortmund mjerumani Mario Gotze, 26. Dortmund wanataka pauni milioni 18 kwa mchezaji huyo wa miaka 26 licha ya Everton na West Ham pia kummezea mate. (Mirror)

Chelsea wamekataa ofa ya pauni milioni 18 kutoka Arsenal kwa mlinzi wa Brazil David Luiz, 31. (Le 10 Sport - in French)

West Ham wanatathmini kumwinda mlinzi wa Manchester United mwenye miak 29 Chris Smalling. Meneja mpya Manuel Pellegrini amepewa bajeti ya pauni milioni 70 kununua wachezaji. (Metro)

West Ham pia wanakaribia kumsaibi mlinzi wa England Alfie Mawson, 24, na kipa wa Poland Lukasz Fabianski, 33, kutoka Swansea. Awali Swansea walikataa ofa Kutoka West Ham kwa wachazaji hao wote. (Sky Sports)

West Ham pia wametoa ofa ya pauni milioni 25 na nyongeza ya miloni 5 kwa wing'a wa Lazio raia wa Brazil Felipe Anderson, 25. (Mail)

Juventus wanapanga kumtafuta mlinzi wa Crystal Place mholanzi Patrick van Aanholt, 27, ikiwa MBrazil Alex Sandro, 27, atakamilisha mpango wa kuhamia Manchester United. (Sun)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment