TCRA yafafanua Kuhusu Watumiaji wa Facebook, Twitter, Instagram Kutakiwa Kujisajili - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 17 June 2018

TCRA yafafanua Kuhusu Watumiaji wa Facebook, Twitter, Instagram Kutakiwa KujisajiliMamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema mtumiaji mmoja mmoja wa mitandao ya Facebook, Instagram na Twitter hatakiwi kujisajili.


Taarifa iliyotolewa Juni 16 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba imesema taarifa hizo ni za uongo kwa kuwa mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii hahitaji kusajiliwa na TCRA.


Taarifa hiyo imesema kanuni zinawataka watumiaji wa mitandao kuwajibika kwa maudhui watakayopakia kwenye mitandao hiyo.


Hata hivyo taarifa hiyo imesema wamiliki wote walio na leseni za utangazaji wanaotumia mitambo iliyosimikiwa ardhini (terrestrial) endapo watapenda kutumia mitandao ya kijamii (facebook, instagram na twitter) kurusha maudhui yao kwa lengo la kujisajili, lazima wajisajili kwanza TCRA.


Kilaba amesema mamlaka hiyo itaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaoeneza uongo huo. 

No comments:

Post a Comment