Sugu Ageuka Mbogo Bunge Kisa Wimbo Wake Kufungiwa "Mimi Sio Kama Roma, Naiburuza Mahakamani Basata" - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 20 June 2018

Sugu Ageuka Mbogo Bunge Kisa Wimbo Wake Kufungiwa "Mimi Sio Kama Roma, Naiburuza Mahakamani Basata"

Ikiwa ni siku moja tangu Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutangaza kuufungia wimbo wa Joseph Mbili ‘Sugu’, msanii huyo ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini amesema atatumia mawakili sita kulishtaki baraza hilo.

Sugu amesema hayo leo June 20, 2018 bungeni na kueleza kuwa wimbo huo umefungiwa wakati bado hata haujatoka.

“Wimbo umevuja wao wanatoa statement ya kufungia, hawajawahi hata kuingia studio, hawajui hata gharama. Wanataka wote tuimbe nyimbo za matusi,” amesema.

“Mimi sio kama Roma, naiburuza mahakamani Basata wimbo umevuja mimi sijautoa bado. Nina mawakili sita nitawaburuza mahakamani ndio watakoma

Hata hivyo wakati Sugu akieleza hilo Naibu waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alisema; Wimbo unavuja vipi wakati uko kwenye mitandao, hata mashairi yake ninayo hapa. Nyie wenyewe mlisema Basata wanafungia nyimbo bila taarifa,’.


Wimbo wa Sugu uliofungiwa unaokwenda kwa jina la #219 ambayo ilikuwa ni namba yake kama mfungwa alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi sita gerezani, hata hivyo alikuja kutoka kabla ya kumaliza muda huo.

No comments:

Post a Comment