STARTIMES YAZINDUA WASAFI TV KWENYE KING'AMUZI CHAO - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 19 June 2018

STARTIMES YAZINDUA WASAFI TV KWENYE KING'AMUZI CHAO


Wapenzi wa burudani kote nchini ni wakati wao kufurahia baada ya Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes kutangaza rasmi kwamba chaneli ya Wasafi TV imeanza kuonekana kupitia king’amuzi chake. Uzinduzi wa chaneli ya Wasafi TV kwenye king’amuzi cha StarTimes umefanyika Jumatatu tar 18 katika Hotel ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam.

Sasa chaneli hii mpya ya Burudani itaweza kutazamwa na watu wengi zaidi Tanzania kwa sababu StarTimes ndicho king’amuzi chenye watumiaji wengi zaidi hapa nchini kuliko kingine chochote. 

“kuanzia sasa Wasafi TV itapatikana katika ving’amuzi vyetu vya Antenna, kwa hiyo watumiaji wa Antenna wanaweza kutazama chaneli hii mpya ikiwa na vipindi vipya ambavyo vitatangazwa baadaye. Pia wateja wanaweza kulipia kifurushi chochote cha Antenna kuipata Wasafi TV, unaweza kulipia NYOTA kwa 7000 tu mwezi mzima, MAMBO Tsh 13,000 tu kwa mwezi na UHURU kwa 24,000 tu.

 Wasafi TV kwa sasa inapatikana kwenye Antenna pekee, na muda wowote kuanzia sasa itakuwa tayari kwa watumiaji wa ving’amuzi vya dish pia”, Ndg David Malisa, Meneja Masoko wa StarTimes.

Chaneli ya Wasafi TV kama walivyodhamiria kuleta mapinduzi katika tasnia ya burudani nchini ni dhahiri kuwa king’amuzi cha StarTimes kitasaidia kulifikia lengo hilo, hasa kupitia teknolojia yake ya urushaji wa matangazo ya kidigitali. Itakumbukwa kuwa StarTimes ndiyo walioleta mapinduzi ya kidigitali tangu mwaka 2009.

“Kumekuwa na villio vingi kwa nini Wasafi TV haipo kwenye StarTimes lakini sasa tayari iko ndani ya StarTimes. Wasafi TV inakuja na lengo kubwa la kuwainua vijana tofauti na ambavyo watu wengi wanafikiria. 

Ndoto kubwa walizonazo vijana huko mtaani sasa tunaelekea kuzitimiza. Pia Wasafi TV kitakuwa chombo cha kukuza sanaa nchini, kwa sababu wasanii tunajuana  na ndio tuna uwezo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe”.

Mbali na kutazama chaneli ya Wasafi TV wateja wa StarTimes wanaweza kuendelea kutazama mechi zote za Kombe la Dunia kaatika kiwango safi kabisa cha picha, HD tena kwa lugha ya Kiswahili. Kama alivyoeleza Malisa.

“Huna haja ya kuhangaika na mechi za mgao, ukiwa na StarTimes hutakosa mchezo hata mmoja tena katika picha ang’avu zaidi. Kwa wateja wa dish unaweza kufurahia mechi zote kwa gharama ndogo sana ya Tsh 19,000 pekee”.

Pia mechi zote zinapatikana kwenye App ya StarTimes kwa watumiaji wa simu janja za kiganjani, unaweza kupakua StarTimes App kutoka Play Store ama App Store kisha utalipia Tsh 5000 tu kutazama mechi zote MUBASHARA kwenye simu yako. 

Kuhusu StarTimes
StarTimes ni kampuni ya Matangazo ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia zaidi ya wateja milioni 10 katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa la maudhui lenye chaneli 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu, tamthiliya, michezo, burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na vingine vingi. Matazamio ya Kampuni ni “Kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata, inamudu, inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa Televisheni ya kidigitali”

No comments:

Post a Comment