Snura Aitwa na Basata Abanwa kwa Masaa Matatu - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 20 June 2018

Snura Aitwa na Basata Abanwa kwa Masaa Matatu

Msanii wa muziki Snura Mushi ameingia kwa mara nyingine kwenye anga za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Jumatano hii msanii huyo ameitwa kwenye Baraza hilo kutokana na video yake chafu iliyosambaa mtandaoni inayomuonyesha akicheza jukwaani.

Kikao hicho kimedumu kwa zaidi ya masaa matatu na hata hivyo msanii huyo amekataa kuzungumzia tukio hilo.

Hii ni takribani mara ya pili kwa msanii huyo kuitwa kwenye Baraza hilo ambalo limewahi kufungia ngoma yake ya ‘Chura’.

No comments:

Post a Comment