REFA AMUOMBA JEZI RONALDO WAKATI MECHI IKIENDELEA - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 22 June 2018

REFA AMUOMBA JEZI RONALDO WAKATI MECHI IKIENDELEA


Refa Mark Geiger aliyechezesha mchezo wa Kundi B Kombe la Dunia juzi Juni 20, 2018 kati ya Morocco dhidi ya Ureno amedaiwa kumuomba jezi mwanasoka bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo wakati mchezo ukiendelea.

Madai hayo yametolewa na kiungo wa Morocco, Nordin Amrabat anayechezea Watford ya England, ambaye alicheza jana licha ya kuumia kwenye mchezo wa kwanza, na  timu yake ilichapwa 1-0 kwa bao pekee la Ronaldo.

“Sifahamu alikuwaje, lakini alikuwa anavutiwa mno Cristiano Ronaldo, na nilimsikia Pepe anasema kwamba alimuomba jezi (Ronaldo) kipindi cha kwanza,” amesema Amrabat Nyota wa Real Madrid.

Ronaldo juzi amefunga bao lake la nne katika mashindano hayo baada ya mechi mbili, Ureno ikifikisha pointi nne sawa na Hispania na kuongoza pamoja Kundi B.

Kutoka Global Publishers

No comments:

Post a Comment