REAL MADRID YAMPIGA CHINI DE GEA, YASAJILI KINDA HUYU KUTOKA UKRAINE - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

REAL MADRID YAMPIGA CHINI DE GEA, YASAJILI KINDA HUYU KUTOKA UKRAINE


Klabu ya Real Madrid imeingia mkataba wa miaka 6 na kinda Andriry Lunin kutoka Zorya Luhansk ya Ukraine.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, amejiunga na Madrid kwa lengo la kumpiga tafu kipa wa sasa Keylor Navas

Madrid imeendelea na usajili huo baada ya kumalizana na kinda mwingine Rodrygo Goes kutoka Santos FC ya Brazil.

Kocha Mkuu mpya wa kikosi cha Madrid ameamua kuanza kukisuka upya kikosi chake baada ya Zinedine Zidane kuondoka.

Ujio wa Luhansk unaweza ukawa umefuta rasmi ndoto za Madrid kuendelea kumuhitaji kipa wa Manchester United, David de Gea ambaye walikuwa wanampigania kwa udi na uvumba.

No comments:

Post a Comment