RC.AYOUB MOHAMMED ATUMA SALAMU ZA EID KWA WANANCHI. - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 14 June 2018

RC.AYOUB MOHAMMED ATUMA SALAMU ZA EID KWA WANANCHI.


MKOA MJINI MAGHARIB SALAMU ZA EID  
SERIKALI YA MKOA WA MJINI MAGHARIBI IMEELEZA KUWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VITAENDELEA KUIMARISHA ULINZI NA KUWADHIBITI WATU WATAKAOKIUKA SHERIA NA TARATIBU ZILOWEKWA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA SIKUKUU YA EID EL FITRI INAYOTARAJIWA KUANZA BAADAE WIKI HII.

AKITOA SALAMU ZA EID EL FITRI ZA MKOA HUO OFISINI KWAKE VUGA, AMESEMA HATUA HIYO IMELENGA KUONGEZA UTULIVU, AMANI NA MSHIKAMANO MIONGONI MWA WANANCHI WA MKOA HUO NA KUWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI ILI KUEPUSHA MADHARA YA MALI NA MAISHA YAO.
AIDHA MHESHIMIWA AYOUB AMEWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI HASA VYA ABIRIA KUZINGATIA KANUNI NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI,NA  ABIRIA WAO NA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KWA KUFUATA MAELEKEZO YATAKAYOTOLEWA NA VYOMBO VYA USALAMA BARABARANI AMBAVYO VITAONGEZA MARADUFU USIMAMIZI NA HAVITOSITA KUWACHUKULIA HATUA WALE WATAKAOKIUKA SHERIA
.
AMESEMA UZOEFU UNAONESHA KUWA KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU BAADHI YA WATU HUTUMIA VYOMBO VISIVYORUHUSIWA KISHERIA KUTEMBEA BARABARANI KWA AJILI YA KUCHUKUA FAMILIA ZAO AU ABIRIA NA BAADHI YA MADEREVA NA MAKONDAKTA KUONGEZA VIWANGO VYA NAULI JAMBO ALILOLITAKA KUACHWA ILI KUTOA NAFASI KWA WANANCHI KUSHEHEREKEA VYEMA SIKUKUU HIYO.

AMEWAOMBA WAZAZI NA WALEZI KUONGEZA UANGALIZI WA WATOTO WAO KWA KUTOWAACHA KWENDA PEKE YAO KATIKA MAENEO YA VIWANJA VYA SIKUKUU ILI KUPUNGUZA MATUKIO YA KUPOTEA NA KUFANYIWA VITENDO VYA UDHALILISHAJI HUKU AKIWAHIMIZA WANANCHI WOTE KUENDELEA KUONYESHA UKARIMU NA UPENDO KWA WAGENI KAMA ILIVYOKUWA NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI. KATIKA HATUA NYENGINE MKUU WA MKOA ALIWAPONGEZA WANANCHI WA MKOA HUO KWA KUTII TAMKO ALILOLITOA KABLA YA KUANZA KWA MWEZI HUO LA KUWAOMBA WAUMINI WA KIISLAMU NA WASIOKUWA WAISLAMU KUWA WASTAHAMILIVU KATIKA KIPINDI CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN KWA KUACHA KUUZA NA KULA CHAKULA WAKATI WA MCHANA KATIKA MIKAHAWA, MAGENGE NA MAENEO YA WAZI JAMBO AMBALO ALISEMA LILIONGEZA HALI YA UVUMILIVU WA KIDINI MIONGONI MWA WANANCHI WA MKOA HUO NA SEHEMU NYENGINE NCHINI.
AKIZUNGUMZIA VIWANJA NA MAENEO YATAKAYOTUMIKA KWA AJILI YA SHEREHE HIZO, MKUU WA MKOA AMEWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA NA SHUGHULI ZA MICHEZO NA SANAA KATIKA VIWANJA HIVYO KUZINGATIA MARUFUKU YA UPIGWAJI WA MUZIKI KATIKA VIWANJA VYOTE VYA SIKUKUU NA KUZINGATIA

KANUNI ZA AFYA KAMA ZITAKAVYOTOLEWA NA MABARAZA YA MANISPAA YA MKOA HUO. AMEVITAJA VIWANJA VITAKAVYOTUMIKA KATIKA WILAYA YA MJINI NI KUWA NI VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, KIBANDAMAITI, KARIAKOO, MNARA WA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI, JAMHURI GARDEN NA FORODHANI PARK NA KWA UPANDE WA WILAYA YA MAGHARIBI “A” NI VIWANJA VYA DOLE SKULI, KIHINANI

MELINANE, SKULI YA MBUZINI, SKULI YA MAANDALIZI MFENESINI, ZANZIBAR PARK, GARAGARA, KIJICHI KWAGUBE, STELLA DARAJABOVU, KIHINANI ZANTEL, SKULI YA REGEZAMWENDO, MWAKAJE UWANJA WA MPIRA. KWA UPANDE WA WILAYA YA MAGHARIBI “B” MHESHIMIWA AYOUB AMEVITAJA VIWANJA HIVYO KUWA NI SKULI YA BIASHARA MOMBASA, MAGEREZA, MAUNGANI, KWA BWAMGENI PANGAWE,

KIEMBESAMAKI KWA ABDALLAH RASHID, KINUNI, NYARUGUSU, MAGIRISI, SKULI YA KWARARA PROGRESSIVE NA FUMBA MAENEO YA UWEKEZAJI WA MJI MPYA WA KISASA UNAOJENGWA NA MWEKEZAJI SAID SALI BAKHRESA. AMEFAFANUA KUWA BAADHI YA VIWANJA HIVYO VITAFUNGULIWA KUANZIA SAA 10:00 JIONI HADI SAA 4:00 USIKU NA VYENGINE VITAFUNGWA SAA 1:00 USIKU KUTOKANA NA SABABU

MBALI MBALI ZIKIWEMO ZA KIUSALAMA WA MAENEO HUSIKA NA KWAMBA KUMBI MAALUM ZILIZORUHUSIWA KUPIGA MUZIKI ZINATAKIWA KUFANYA HIVYO KUANZIA SAA 2:30 HADI SAA 6:00 USIKU. SIKUKUU YA EID EL FITRI INASHEHEREKEWA KILA MWAKA MARA BAADA YA WAISLAMU KUKAMILISHA MOJA YA NGUZO YA KIISLAMU YA FUNGA AMBAPO KWA MWAKA HUU SALA YA EID EL FIRTI ITAFANYIKA KATIKA

VIWANJA VYA MAISARA SULEIMAN KUANZIA SAA 1:00 ASUBUHI ITAKAYOFUATIWA NA BARAZA LA EID LITAKALOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA SHEIKH IDRISSA ABDULWAKIL KIKWAJUNI MAARUFU BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZAMANI.

NA FATUMA MOHAMMED

No comments:

Post a Comment