RAMOS AMPONDA MARADONA KIANA, AWAAMBIA ARGENTINA BORA ZAIDI KWAO NI MESSI - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 21 June 2018

RAMOS AMPONDA MARADONA KIANA, AWAAMBIA ARGENTINA BORA ZAIDI KWAO NI MESSI
Beki Sergio Ramos ni mgumu hasa na kwa maneno hajambo, kwani safari hii ameamua kumtuoia dongo, gwiji Diego Maradona huku akiwakumbusha wapenda soka wa Argentina kuwa Lionel Messi ni zaidi ya Maradona.


Baada ya Messi kukosa mkwaju wa penalti katika Kombe la Dunia, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa raia wa Argentina wakiona kuwa hakufanya vema.


Lakini Ramos amesema Messi ni bora zaidi ya Maradona katika historia ya soka la Argentina na wapenda soka waelewe.

Akizungumza jana mara baada ya mechi yao ya Kombe la Dunia dhidi ya Iran, Ramos alionyesha wazi akimjibu Maradona ambaye alisema kuwa Ramos si kiongozi bora katika timu kama ilivyo kwa Diego Godini wa Uruguay.

“Kwangu Messi ni bora zaidi katika historia ya soka la Argentina, Maradona ilikuwa ni kabla ya Messi, wakati huo na sasa ni mambo tofauti.

“Kama Messi anakosea inatokea katika mpira lakini ukiangalia kwa ubora hakuna anayemfikia katika historia ya soka la nchi hiyo,” anasema.

No comments:

Post a Comment