Polisi Tabora yawakamata majambazi 5 - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 12 June 2018

Polisi Tabora yawakamata majambazi 5

Ikumbukwe kwamba tukio la kuvamiwa mfanyabiashara huyu aitwaye OMARY RAMADHAN KWAYI  lilitokea tarehe  31/05/2018 saa 19:38hrs  huko maeneo ya mtaa wa Mwayunge  wilaya ya Igunga Mkoa wa TABORA ambapo majambazi yalimvamia nyumbani kwake na kumpora pesa taslimu Tshs 39,800,000/=  pamoja na simu aina ya TECNO yenye thamani ya Tsh 370,000/=

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Tabora lilifanya uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata majambazi watano ambao walikutwa wakiwa na mali mbalimbali ambazo ziliibwa katika tukio hilo

Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi  Mkoa wa  Tabora SACP WILBROD MUTAFUNGWA amewataja majambazi hao kwa majina ya  MSABAHA RAMADHANI HASSAN, Miaka 32,Mkazi wa Igunga huyu ni ndugu wa Mfanyabiashara huyo, IBRAHIMU MUHAMED, Miaka 38 huyu ni Mfanyabiashara mwenzie, KISUDA RAMADHAN HASSAN, Miaka 40, Mkazi wa Manyoni huyu ni Kaka yake na Mfanyabiashara huyo, MBOYI KISUDA, Miaka 28, Mkazi wa Manyoni na  GODFREY NJAU,Miaka 33, Mkazi wa manyoni.

Majambazi hao wamekamatwa na  Pesa kiasi cha Tshs 4,600,000/= pamoja na simu aina ya TECNO ambayo ni mali ya mfanyabiashara huyo ambayo nayo iliibiwa katika tukio hilo.

Kwa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora amesema watuhumiwa wote watano wamehojiwa na wamekiri kuhusika na tukio hilo na juhudi zinaendelea ili kuweza kuzipata pesa nyingine zilizoibwa.

No comments:

Post a Comment