PICHA:AFRIKA KUNAFANANA, TUNISIA YAPOTEZA, YACHAPWA MABAO 2-1 NA ENGLAND, KANE AMALIZA KAZI DAKIKA YA 90 - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 18 June 2018

PICHA:AFRIKA KUNAFANANA, TUNISIA YAPOTEZA, YACHAPWA MABAO 2-1 NA ENGLAND, KANE AMALIZA KAZI DAKIKA YA 90


England imekusanya pointi zote tatu katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia 2018 baada ya kufiunga Tunisia kwa mabao 2-1.

Mabao mawili ya Harry Kane, la kwanza katika dakika ya 11 na lile la pili dakika ua 90 ndiyo yameipa ushindi England.


Ilionekana wazi tokea dakika ya 70 kuwa Tunisia walikosea zaidi kulinda kwa muda mrefu huku wakiwa na mashambulizi machache.


Mara kadhaa, England walipoteza nafasi nyingi za kufunga huku Tunisia wakishambulia kwa kushitukiza.

Tunisia imekuwa timu ya nne ya Afrika kupoteza mechi mechi ya kwanza na kesho ni zamu wa Senegal. Hata hivyo, Tunisia pia imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kufunga bao katika Kombe la Dunia 2018.
No comments:

Post a Comment