Panya Wavamia ATM na Kutafuna' Pesa - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 20 June 2018

Panya Wavamia ATM na Kutafuna' Pesa

Mafundi waliofika kuukarabati mtambo wa ATM ambao ulikuwa umeharibika katika jimbo moja nchini India walipigwa na butwaa walipoufungua kubaini tatizo lilikuwa wapi.

Noti za thamani ya rupia 1.2m (£13,300; $17,600) zilikuwa zimechanwa na kuraruliwa na panya katika benki hiyo jimbo la Assam.

Polisi wanasema panya hao pengine waliiingia ndani ya mtambo huo kwa kupitia kwenye tundu lililokuwa litumiwe kuingizia nyaya, gazeti la Hindustan Times limeripoti.

Afisa wa polisi Prakash Sonowal alisema kwamba mtambo huo umekuwa haufanyi kazi kwa siku 12 hizi, gazeti la Hindustan Times limeongeza.

Mhubiri awaomba waumini wamnunulie ndege Marekani
Mafundi waliofungua mtambo huo walipata noti za rupia 2,000 na rupia 500 zikiwa zimeharibiwa.

Walifanikiwa kunusuru noti za jumla ya thamani ya rupia 1.7 milioni, maafisa wanasema.

No comments:

Post a Comment