Nywele za beki wa zamani wa Barcelona, Carles Puyol zamkosesha dili la mamilioni nchini Iran - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 25 June 2018

Nywele za beki wa zamani wa Barcelona, Carles Puyol zamkosesha dili la mamilioni nchini Iran

Beki kisiki wa zamani wa Barcelona na Timu ya taifa ya Hispania, Carles Puyol amekosa dili la kuchambua michezo ya kombe la Dunia katika kituo cha runinga cha IRTV 3 cha nchini Iran kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni kutokana urefu wa nywele zake.

Carles Puyol
Puyol ambaye wiki iliyopita alialikwa kuchambua mchezo kati ya Hispania na Iran lakini hakuruhusiwa kuingia kwenye studio za kituo hicho cha runinga zilizopo mjini Tehran kufanya uchambuzi wa mchezo huo.
Taarifa kutoka Mtandao wa habari wa  Entekhab wa nchini Iran, umeleeza kuwa staili ya kuweka nywele ndefu ni staili yenye mkanganyiko  nchini Iran na inapingana na baadhi ya sheria za kiislamu.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mara moja alikatazwa kuingia kwenye studio za kituo hicho cha runinga kwa sababu ya urefu wa nywele zake.
Hata hivyo, nchini Iran hakuna sheria rsmi inayozungumzia mitindo ya nywele inayoruhusiwa na isiyoruhusiwa ingawaje imeelezwa kuwa kuna sera ya kuzuia kueneza tamaduni za kigeni nchini humo kupitia vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment