Nimetulia Sina Papara Mungu Yupo Lazima Niolewe na Daimond- Lynn - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 13 June 2018

Nimetulia Sina Papara Mungu Yupo Lazima Niolewe na Daimond- Lynn

VIDEO Queen Irene Charles ‘Lynn’ ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema ametulia na hana papara kwani kama Mungu amepanga aolewe na msanii huyo, lazima itokee!

Akizungumza na Risasi Jumatano, Lynn alisema, hawezi kuleta drama kwenye mitandao kuhusiana na suala lake na Diamond ila anachojua yeye kama Mungu amepanga aolewe naye, itakuwa hivyo na kama siyo basi ataolewa na mwingine aliyepangiwa.

“Unajua siku zote ndoa hupangwa na Mungu hivyo kama Dai (Diamond) alipangwa kuwa wangu basi atakuwa wala sina papara, kama hajapangwa kuwa wangu atakuja mwingine,” alisema Lynn.

No comments:

Post a Comment