Ngoma mpya ya Sugu yakutana na rungu la Basata - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 19 June 2018

Ngoma mpya ya Sugu yakutana na rungu la BasataBaraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa #219 ulioimbwa na Mbunge Joseph Mbilinyi 'Sugu' kwa madai kwamba una maneno ya uchochezi na kuhatarisha amani na utengano miongono kwa jamii. 

Taarifa kutoka BASATA inasema kwamba wamekuwa wakipokea simu za malalamikp kadhaa kutoka kwa wadau ambao wamechukizwa na wimbo huo ambao si tu kutokana na umaneno ya kichochezi bali pia kutofuata taratibu za utoaji wa wimbo kwa umma hali inayopelekea kuhoji weledi na hadhi ya msanii. 

Katibu Mtendaji wa BASATA, Ngereza amesema kuwawasanii wengi wanafanya sanaa kuburudisha na kuelimisha lakini hawapo tayari kuvumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza sekta ya sanaa kama kichaka cha kusambaza sumu kwa lengo la kuigawa jamii na kuharibu amani na utulivu. 

Mbali na kuufungia wimbo huo, BASATA imemuonya Sugu kuacha mara moja kujihusisha kwa namna yoyote ya kuutangaza au kuusambaza wimbo huo.

No comments:

Post a Comment