NAIBU SPIKA BARAZA LA WAWAKILISHI AWATAKA WANAWAKE KUSHIRIKI MASUALA YA UONGOZI ILI KUWEZA KUJITETEA - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 18 June 2018

NAIBU SPIKA BARAZA LA WAWAKILISHI AWATAKA WANAWAKE KUSHIRIKI MASUALA YA UONGOZI ILI KUWEZA KUJITETEA

   Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh.Mgeni Hassan Juma amewataka Wanawake kuwacha woga na badala yake washiriki katika masuala ya siasa na Uongozi ili waweze kutetea masuala yao katika ngazi za maamuzi.
    Amesema iwapo Wanawake watakuwa na woga na hawatosimama kugombea nafasi za uongozi zinazokuwepo na Wanawake wenzao kuwaunga mkono mataizo walionayo hayatoweza kuondoka.
    Akizungumza na wanachama na Viongozi wa Kikundi cha Nuru njema Jangombe Wilaya ya Mjini amesema kitendo cha baadhi ya Wanawake kujiweka nyuma katika masuala ya kimaendeleo kinawakosesha fursa ya kuelezea masuala yanayowahusu katika ngazi husika.
   Mh. Mgeni ambae pia ni Mwakilishi wa Viti maalumu kupitia Wanawake Mkoa wa Mjini  amesema Wanawake iwapo watajikusanya na kuwa kitu kimoja wataweza kuepukana na tatizo la umasikini  kwani Wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika Maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
     Mbali na hayo  amewataka Wanawake wenzake wasivunjike moyo na badala yake washirikiane katika harakati za kimeendeo licha ya matatizo mbali mbali walionayo.
   Akielezea kuhusu uchumi amewataka wanawake kuhamasishana na kujiunga katika Vikundi vya ushirika ili waweze waweze kuweka akiba itakayowasaidia katika maisha na kuepukana na hali ya utegemezi.
   Amesema ili kuweza kufikia maelendo hayo hakuna budi kwa Wanawake  kuhurumiana na kupendana hasa ukichukulia tatizo la Mwanamke mmoja ni tatizo la Wanawake wote.
    Mbali na hayo amewahimiza wanaokopa kutosahau kulipa kwa wakati ili na wenzao waweze kuchukuwa na kuwaendesha katika maisha  na kuweza kufikia malengo ya serikali ya kuanzisha vikundi vya ushirika.
     Amesema hakuna Dini yoyote Duniani inayokubali Watu kukopa bila kulipa hivyo kufanya kinyume ni dhambi  na kuitaka jamii kubadilika kwa kujiaminisha kwa wale wanaowaamini.
    Hata hivyo amesema kauli mbiyu ya sacosi ya ushirika inasemasema weka zaidi, kopa zaidi na lipa kwa wakati ili na wengine wafaidike na Mikopo hiyo jambo ambalo linapaswa kutiliwa mkazo na Wanaushirika.
    NA TAKADIR,ALI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment