Nahreel Sasa Kufanya Kazi na Keri Hilson Pamoja na Akon - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 19 June 2018

Nahreel Sasa Kufanya Kazi na Keri Hilson Pamoja na Akon

Ukitaja waandaaji wa muziki waliofanya ngoma kubwa nchini Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo huwezi kuuacha kumtaja Nahreel kutoka studio za The Industry.

Sasa ukweli ni kwamba licha ya kufanya ngoma nyingi za wasanii wakubwa barani Afrika akiwemo Mr. Eazi na Patoranking, tayari mkali huyo wa midundo ameshafanya kazi na Akon na Kery Hilson.
Akithibitisha taarifa hizo mzazi mwenzie wa kundi la Navy Kenzo, Aika amesema kuwa tayari Nahreel ameshamaliza kufanya kazi hizo na kinachosubiriwa ni muda tu.
“Kuna meneja wetu mmoja nchini Marekani ambaye amejaribu kumfanya Nahreel afanye kazi na Akon.. na Kery Hilson soo! Nahreel soon anafanya nao kazi,“amesema
Kama ulikuwa hujui basi nikujuze, kuwa Nahreel ana mtoto mmoja anaeitwa Gold ambae amezaa na mpenzi wake wa muda mrefu na mwanamuziki mwenzake ambae wameunda kundi linaloitwa NAVY KENZO

No comments:

Post a Comment