Nabii wa kujitawaza ataka Milioni 4 ili Nigeria Ishinde Kombe la Dunia - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

Nabii wa kujitawaza ataka Milioni 4 ili Nigeria Ishinde Kombe la DuniaNabii wa kujitawaza nchini Nigeria anayejulikana kama Tommy Yisa Aika amewataka waumini wake wamlipe kiasi cha naira 750,000 sawa na zaidi ya Milioni 4 za Kitanzania ili atume kikosi chake cha mashujaa wa maombi kiwasaidie timu ya taifa ya Nigeria kushinda kombe la dunia nchini Urusi.

Kwa upande mwingine Nabii huyo alisema kuwa timu hiyo ya taifa ya Nigeria ilipokea kichapo kutoka kwa Croatia kwa sababu Mungu alikuwa anaawadhibu kwa kumchagua kocha mzungu ambaye ni Gernot Rohr.

Katika mechi hiyo Nigeria walichapwa 2-0 na Croatia ambayo ndio ilikuwa mechi yao ya kwanza katika Kombe la Dunia Urusi.


Aidha Nabii huyo amesema kuwa waumini wake maalum wako tayari kuanza kazi na kurekebisha kosa walilolifanya na kupata neema ya Mungu katika michuano hiyo.

Nigeria watakutana na Argentina katika mechi yao ya mwisho Kundi D na ndio itakayoamua hatma ya timu hiyo kusonga mbele katika michuano hiyo

No comments:

Post a Comment