Mzee Majuto- Mimi Sijafa Ila Mungu Akinichukua Mniombee Niende Mahali Pazuri - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 26 June 2018

Mzee Majuto- Mimi Sijafa Ila Mungu Akinichukua Mniombee Niende Mahali Pazuri

BAADA ya kusambaa kwa taarifa katika kimtandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Muigizaji Mkongwe nchini, Mzee Amri Majuto, amezungumza na kuwahakikishia Watanzania kwamba yeye ni mzima wa afya na anaendelea na matibabu yake baada ya kurejea kutoka India.Akizungumza na Global TV Online, mzee Majuto amewataka Watanzania wote waendelee kumuoombea ili afya yake irejee huku akiipongeza serikali kwa kumsaidia kwenda kutibiwa India.

“Niwaambie Watzania kwamba wasishtuke mimi sijafa, ni mzima jamani, kama Mwenyezi Mungu atanichukua, basi mje mnizike kwa wingi, mniombee niende mahali pazuri. Mlimpenda sana rafiki yenu Kanumba lakini Mungu akampenda zaidi,” amesema Mzee Majuto.

Taarifa za kuzushiwa kifo kwa mkongwe huyo zimeanza kusambaa mapema leo Juni 26, 2018 asubuhi ambapo mwanaye, Hamza Majutio alikanusha taarifa hizo na kusema mzee wake huyo ni mzima wa afya ana anaendelea na matibabu nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment