Mzee Majuto Arejea Nchini Akitokea Katika Matibabu India - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

Mzee Majuto Arejea Nchini Akitokea Katika Matibabu India

Msanii wa filamu Bongo, Mzee Majuto amerejea nchini akitokea katika matibabu nchini India.

Mara baada ya kutoa nchini Mzee Majuto amesema hali yake ya kiafya imetengamaa ukilinganisha na hapo awali. Hii ni kutokana na huduma alizopatiwa ambazo ameeleza ni za kisasa zaidi ukilinganisha na za hapa nchini.

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa anahitaji kupumzika zaidi na hana mpango wa kurejea katika sanaa ya maigizo.

Mzee Majuto aliondoka nchini May 4, 2018c kuelekea India. April 28, 2018 alirudishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo awali alikuwa akipatiwa matibabu kabla ya kuhamishiwa hopitali ya binafsi, Tumaini, ndipo akapelekwa India.

No comments:

Post a Comment