Mwigulu ajibu wanaoibeza na Kusema Bajeti ya Mwaka Huu ni 'Bajeti Hewa' - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 18 June 2018

Mwigulu ajibu wanaoibeza na Kusema Bajeti ya Mwaka Huu ni 'Bajeti Hewa'Serikali ya awamu ya tano kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema wanaobeza Bajeti ya mwaka 2018/2019 ni hewa hawaelewi maana halisi ya Bajeti yenyewe.


Mh. Mwigulu ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya kwanza ya vijana wa Chama cha Mapinduzi wa vyuo vikuu vya Mkoa wa Kilimanjaro na kusema kuna watu wameibuka wakidai Bajeti ya serikali ya mwaka 2018/2019, ya Shilingi trilioni 32.47 iliyowasilishwa Juni 14 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ni hewa jambo ambalo si sahihi.


"Haijawahi kutokea Bajeti ya Maendeleo kuwa hewa, hivyo wanaozungumza na kujadili kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni hewa hawaelewi maana halisi ya Bajeti", amesema Mwigulu.


Kwa upande mwingine, Mwigulu amesema kuwa ni lazima kufunga mkanda na kujenga misingi itakayoiwezesha nchi kusimama na kujitegemea

No comments:

Post a Comment