Mwanamke Auawa na Kumezwa na Chatu - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 19 June 2018

Mwanamke Auawa na Kumezwa na Chatu

Mwanamke mmoja nchini Indonesia ameuawa na kumezwa mzima mzima na chatu mwenye urefu wa mita 7.

Licha ya visa kama hivyo kuwa vichache hiki ndicho kisa cha hivi karibuni cha mtu kuliwa na chatu nchini Indonesia kwa takriban mwaka mmoja.

Ni kipi kilimpata mwanamke huyo?
Wa Tiba, 54, alitoweka Alhamisi iliyopita wakati akiwa kwenye shamba lake la mboga katika kisiwa cha Muna mkoa wa Sulawesi. Shughuli kubwa ya kumtafuta ilifanywa na wakaazi wa eneo hilo.

Viatu vyake na upanga vilipatikana siku moja baadaye huku chatu aliyekuwa na tumbo lililofura akipatikana mita 30 kutoka eneo hilo.

Mwanamume aliyetoweka apatikana ndani ya chatu Indonesia
Wenyeji walishuku kuwa nyoka huyo alimuua, kwa hivyo wakamuua na kumtoa shambani.

Tumbo la nyoka huyo lilipasuliwa na mwili wa mwanamke huyo ukapatikana ndani.

Picha za kutisha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Indonesia zikionyesha mwili wa mwanamke huyo ukitolewa tumboni mwa chatu huyo mbele ya umati mkubwa.

Chatu wanashambuaje?
Chatu wa sulawesi wanaweza kukua hadi urefu wa miaa 10 na wana nguvu sana, Wanashambulia kwa kuvizia, wakijifungia kwa windo lao na kulivunja kwa kufinya hadi kuua.

No comments:

Post a Comment