MWAKILISHI WA JIMBO LA PONGWE AKEMEA TABIA YA BAADHI YA WANACHI KUHARIBU MIUNDOMBINU ZA SERIKALI - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 26 June 2018

MWAKILISHI WA JIMBO LA PONGWE AKEMEA TABIA YA BAADHI YA WANACHI KUHARIBU MIUNDOMBINU ZA SERIKALI

Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Mh. Mwalimu Juma Mwalimu amekemea tabia ya baadhi ya Wananchi kufanya uharibifu wa miondominu ya serikali na kuwataka wananchi kuacha muhali na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili wachukuliwe hatua.
   Amesema Serikali imekuwa ikitumia pesa nyingi kwa ajili ya kutengeneza au kuboresha miondombinu ikiwemo ya elimu, afya, maji safi na barabara  lakini kitendo cha baadhi ya wananchi kufanya uharibifu wa kuikata kwa makusudi  na kujitokeza baadhi ya watu na kufanya uharibifu kimekuwa kikirudisha nyuma juhudi za serikali .
   Akizungumza na Uongozi wa Skuli ya Kijitopele “B” wakati alipofanya ziara ya kukagua,mara  baada ya kuibiwa kwa masinki 3 ya vyoo katika Skuli hiyo wakati wa kufanya ukarabati ukiwa unaendelea amesema ni jambo la kusikitisha kuona miondombinu ya serikali inafanyiwa uharibifu huku wananchi wamekuwa wakiwatizama tu wahalifu hao na kushindwa kuwapeleka katika vyombo vya sheria jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa hali na mali.
  Aidha amewataka Vijana kujishughulisha kufanya kazi za halali na kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya na bangi, wizi na ubakaji.

   Hata hivyo Mh. Khamis  amesema Uongozi wa Jimbo unakusudia kujenga Uzio ili kuwanusuru na vitendo vya uharibifu wa miondombinu ya Skuli hiyo na kuwaomba Wananchi kutoa mashirikiano ya kutosha katika kupiga vita suala hilo.

    Nae Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kijito upele “B” Makame Hana Ali amesema tukio hilo limetokea juzi baada ya mtuhumiwa  Ibrahim Omar Hamad maarufu ‘’Gombe’’mwenye umri wa miaka 19,mkaazi wa Kijitoupele kuvunja milango na kuiba masinki ya matatu ya vyoo na kuwapa usumbufu mkubwa waalimu na wanafunzi wanapotaka kuenda kujisaidia.
    
   Amesema hali hiyo imewapa usumbufu wanafunzi na Waalimu kwa kutumia kutumia vyoo kidogo ambavyo havitoshelezi na kulazimika kutumia nyumba za jirani na kuhofu kutokea kwa maradhi ya mripuko ikiwemo kipindupindu na matumbo ya kuharisha hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea.
  Mwalimu Hana amesema amesema mara baada ya kupata malalamiko hayo wameyafikisha malalamiko yao katika kituo cha Polisi Kijitoupele na tayari  limeanza kulifuatia suala hilo.

No comments:

Post a Comment