Mume Amuua Mkewe kwa Kumchoma Kisu naye Ajiua - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 20 June 2018

Mume Amuua Mkewe kwa Kumchoma Kisu naye Ajiua

Mwanaume mmoja amuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake kisha na yeye mwenyewe kujichoma kisu tumboni na kufariki dunia wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea katika nyumba za kulala wageni ya 'Angel Guest House' iliyopo kijiji cha Kanyara Wilayani Sengerema mkoani Mwanza ambapo wanandoa hao walifikia kwaajili ya mapumziko.

Aidha, Kamanda Msangi amesema inadaiwa kuwa wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu katika familia yao, hali iliyopelekea mwanamke kuondoka nyumbani kwao kijiji cha Bukokwa kisha kwenda kupumzika kwa wakwe zake kijiji cha Kanyara.

Msikilize hapa chini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi akielezea kiundani juu ya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment