MSANII HUYU WA KIKE BONGO AMFUATA SALAH URUSI - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

MSANII HUYU WA KIKE BONGO AMFUATA SALAH URUSI


Staa wa Kibao cha Ninogeshe, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema uwezo mkubwa wa mshambuliaji Mohammed Salah ndiyo uliomfanya yeye akaishabikia timu ya Taifa ya Misri kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko nchini Urusi.

Misri tayari imetolewa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa mechi mbili za awali na sasa imebakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba dhidi ya Saudi Arabia.

Nandy anayesifika kwa sauti nzuri, alisema licha ya kufanya muziki kingine kinachomvutia ni uwezo wa Salah ambaye ndiye staa wa Misri na Klabu ya Liverpool hivyo anapenda kumuangalia anapokuwa uwanjani.

“Kwa mbali sana huwa nafuatilia masuala ya michezo, huyu mchezaji anayetumikia timu ya Misri, Salah ananikosha sana kwa kuwa mimi pia ni shabiki wa klabu yake ya Liverpool, hivyo kanipeleka moja kwa moja Urusi ambako mashindano yanafanyika, namkubali kweli,” alisema.

No comments:

Post a Comment