Msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM-Taifa(UVCCM) Wapata Ajali - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 10 June 2018

Msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM-Taifa(UVCCM) Wapata AjaliSIMIYU: Msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM-Taifa(UVCCM), Kheri D. James wapata ajali wilayani Meatu baada ya gari la Polisi lililokuwa kwenye msafara huo kuchomoka tairi

Inadaiwa baada ya kupasuka tairi gari hilo limeziba njia na hivyo kusababisha magari ya nyuma yake kugongana ambapo basi la Rombo limegonga gari lililokuwa limebeba madiwani

Mpaka sasa hakuna taarifa ya kifo lakini inaelezwa kuwa Majeruhi watatu wamekimbizwa katika hospitali ya Mwandoya kwa matibabu

Hali ya Kheri James pamoja na Maafisa toka makao Makuu waliofuatana nae ziko imara bila jeraha lolote isipokuwa kuna baadhi ya Madiwani wamepata majeraha

No comments:

Post a Comment