Mohamed Salah apewa uraia wa heshima Chechnya - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 25 June 2018

Mohamed Salah apewa uraia wa heshima Chechnya


Kiongozi wa Chechnya, Ramzan Kadyrov ametangaza kumpatia uraia wa heshima wa Urusi mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah.

Mohamed Salah yuko nchini Urusi kwenye michuano ya kombe la dunia akiiwakilisha Misri, ambaye kambi yake ya mazoezi ipo mjini Grozny, Chechnya.

Kadyrov amekuwa akikosolewa, akishutumiwa kumtumia mchezaji huyo kwa propaganda zake za kisiasa.

Utawala wa Kadyrov umekosolewa kwa kile kinachodaiwa kuwa ukiukaji wa haki za binaadamu, madai ambayo ameyakana wiki iliyopita wakati alipohojiwa na BBC.

"Mohamed Salah ni raia wa heshima wa Chechnya! ndio!” Kadyrov aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Ijumaa.

“Katika hafla ya chakula cha jioni nilipatia heshima hiyo nikampatia Mohamed Salah nakala ya tangazo na beji,” alisema.

Salah alikosa goli wakati wa mchezo kati ya Misri na Uruguay wakati ambapo akiendelea kuuguza jeraha lake la bega.

Hatma ya Mohamed Salah na vuguvugu za siasa 
Taifa hilo la Afrika litacheza na Saudi Arabia mjini Volgograd leo Jumatatu huku nahodha na mshambuliaji hodari wa Misri, Mohamed Salah, anafikiria kustaafu kuitumikia nchi yake mara tu baada ya nchi hiyo kumaliza mechi za makundi za Kombe la Dunia 2018.

Timu zote mbili zitafungasha virago na kureja nyumbani kwani zimepoteza mechi zote mbili za mwanzo hatua ya makundi.

Sababu za Salah kufikia hatua hiyo imeelezwa kuwa ni mambo ya kisiasa ikielezwa watawala wa Misri wamekerwa na ukaribu wake na kiongozi wa Chechnya, Ramzan Kadyrov, ambaye tayari amempa mshambuliaji huyo uraia wa heshima wa Chechnya.

No comments:

Post a Comment