Mkutano wa Trump na Kim Jong Un wafanyika Singapore - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 12 June 2018

Mkutano wa Trump na Kim Jong Un wafanyika Singapore


Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.

Mkutano huo ulianza kwa viongozi hao wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao wakiwa na wakalimani wao, uliochukua dakika 38.


Kwa sasa, viongozi hao wanakula chakula cha mchana.

Baadaye washauri na maafisa mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la nyuklia likitarijiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado makubaliano yatakua yapi.

No comments:

Post a Comment