MKOA WA MJINI MAGHARIBI KULISHUGHULIKIA SUALA LA OMBA OMBA - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 11 June 2018

MKOA WA MJINI MAGHARIBI KULISHUGHULIKIA SUALA LA OMBA OMBA


MKOA WA MJINI MAGHARIBI 
SERIKLAI ya mkoa wa Mjini Magharibi imesema inaendelea kulishughulikia ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo la omba omba wanaoonekana mjini ambao wanaondoa haiba ya nchi na watu wake.
Mkuu wa mkoa huo Ayoub Mohammed Mahmoud ametoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Vuga hivi karibuni na kueleza kwa sasa suala hilo linashughulikiwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mjini ambayo imefanya mawasiliano ya awali na serikali  ya  mkoa wa Dar es salam na mikoa mingine ya Zanzibar ili kuweka utaratibu mzuri wa kuwaondoa na kuwadhibiti omba omba hao.
Amesema utafiti uliofanywa na ofisi yake umebaini kuwepo kwa baadhi ya watu wanaotoka katika mikoa mingine ya Zanzibar na Tanzania bara wanaokwenda mijini kuomba kwa lengo la kujipatia kipato, hivyo kabla ya kuwaondoa itafanya upembuzi yakinifu ili kubaini chanzo cha kufanya shughuli hiyo na namna watakaoweza kuwasaidia kuachana nayo.
Amesema serikali ya zote mbili zimeweka utaratibu mahsusi wa kuwahudumia watu wasiojiweza hivyo kabla ya kuchukua hatua ya kuwaondosha watafanya uhakiki ili kubaini namna bora ya kulishughulikia tatizo hilo kwa lengo la kuwadhibiti wasirudi katika maeneo hayo kama ilivyotokea awali.
Aidha mkuu huyo wa mkoa ameikumbusha jamii kuendelea kutekeleza wajibu wao wa kuwatunza wazee na watu wasiojiweza badala ya kuwatelekeza na kuwataka watu wenye tabia ya kuomba omba licha kupatiwa matunzo na jamaa zao au serikali kuacha kufanya hivyo kwani wanaiabisha nchi na jamaa zao.
Ameongeza kuwa uamuzi wa Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kuanzisha pencheni jamii kwa wazee wenye umri wa kuanzia miaka 70 na uamuzi wa rais wa kwanza wa Zanzibar sheikh abeid aman karume wa kuweka makaazi ya wazee unguja na pemba ulioendelezwa na awamu zote za serikali ya Zanzibar umelenga kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wa Zanzibar na watu wasio na uwezo hivyo jamii inapaswa kuunga mkono juhudi hizo kikamilifu.
Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa amewataka wakaazi wa maeneo mbali mbali ya mkoa huo wanaokabiliwa na ubovu wa barabara kuendelea kuvuta subira wakati serikali kuu na serikali za mitaa zikiendelea kufanya tathmini kabla ya kuzifanyia matengenezo bara bara hizo ambazo baadhi yake zimeharibiwa na mvua za masika zilizomalizika hivi karibuni.
Aida Ayoub amewatoa hofu watumiaji wa barabara ya Kinuni Tundauwa hadi Kinuni Skuli kuwa serikali  inafanya jitihada za kuifanyia matengenezo ya dharura ili iweze kupitika bila ya usumbufu wakati ikilitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo la barabara hiyo ili iendane na ile ya Magogoni – Kinuni – Kijitoupele yenye urefu wa kilomita 3 iliyojengwa kwa kiwango cha lami mwaka uliopita.
Sambamba na hayo mkuu huyo ameelezea juu ya hatu ya serekali za mkoa na wilaya zilipo fikia juu muhanga alie ingiliwa na maji katika nyumba yake wakati wa mvua za masika bibi HALIMA SILAHA MOHAMMED mkazi wa mtoni kitadu amesema kuwa mpaka saa wamefikia pazuri ila wanasubiria taratibu za kisheria kwa kuaza ujenzi kwa mkazi huyo
NA FATUMA MOHAMMED

No comments:

Post a Comment