Misri Yatandikwa Tena Bao 3-1 na Urusi, Kwa Matokeo Haya, Misri ndo Basi Tena!! - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 20 June 2018

Misri Yatandikwa Tena Bao 3-1 na Urusi, Kwa Matokeo Haya, Misri ndo Basi Tena!!Misri Yatandikwa Tena Bao 3-1 na Urusi....Kwa Matokeo Haya, Misri ndo Basi Tena!!

Bigie · 39 minutes agoTimu ya taifa ya Misri huenda ikawa timu ya kwanza kuaga Fainali za Kombe la Dunia, baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo pamoja na kuwa kimahesabu inaweza kuwa bado, lakini kiuhalisia ni ngumu.


Misri ambayo ilifungwa bao 1-0 na Uruguay kwenye mechi yake ya kwanza, leo tena imekubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa wenyeji Urusi hivyo kuwa na hali mbaya katika Kundi A.


Msimamo wa Kundi A lenye timu za Urusi, Saudi Arabia, Misri na Uruguay unaongozwa na wenyeji Urusi wenye alama 6 kwenye mechi mbili wakifuatiwa na Uruguay yenye alama 3 kwenye mechi 1.


Saudi Arabia zinavutana na Misri mkiani ambapo Saudi Arabia imepoteza mechi moja dhidi ya Urusi ilipofungwa mabao 5-0 kwenye mechi ya ufunguzi.


Misri ili isonge mbele inahitaji kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Saudi Arabia kwa kuanzia mabao angalau 5 kwenda juu huku ikiomba Uruguay ipoteze dhidi ya Saudi Arabia kwa idadi ndogo ya mabao. Kiujumla Misri imeaga michuano.

No comments:

Post a Comment