MEXICO YAZIDI KUCHELEA KUNDI F BAADA YA KUWAMALIZA WAKOREA, CHICHARITO ATUPIA - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

MEXICO YAZIDI KUCHELEA KUNDI F BAADA YA KUWAMALIZA WAKOREA, CHICHARITO ATUPIA


Mchezo wa kundi F katika michuano ya Kombe la Dunia Urusi, umemalizika kwa Korea Kusini kufungwa mabao 2-1 na Mexico.

Mabao ya mchezo huo yamewekwa kimiani na Carlos Vela dakika ya 26 kwa njia ya penati pamoja na Xavier Hernandez kwenye dakika ya 66.

Bao pekee la Korea limewekwa kimiani na Song Heung mnamo dakika ya 90 zikiwa zimeongezwa tatu mpira kumalizika.

Mechi nyingine ya kundi F inayosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka duniani, ni baina ya Sweden na Ujerumani itakayoanza saa 3 kamili usiku huu.

No comments:

Post a Comment