MESSI ATOA USHAURI HUU KWA MABOSI WAKE BARCELONA KUHUSIANA NA SALAH - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 17 June 2018

MESSI ATOA USHAURI HUU KWA MABOSI WAKE BARCELONA KUHUSIANA NA SALAH


Imeripotiwa kuwa nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, amewashauri mabosi wake wa klabu yake kumsajili mchezaji wa Liverpool, Mmisri, Mohamed Salah.

Messi amefikia hatua hiyo baada ya mshambuliaji wa Atletico de Madrid, Antoine Griezmann kuamua kubaki na klabu yake ambaye alikuwa anawindwa na Barcelona.

Kufuatia mipango ya Barcelona kushindwa kumpata Griezmann, Messi amewaomba viongozi wake wa juu wafanye harakati za kumsajili Salah ili kuja kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Salah amejizolea umaarufu mkubwa hivi sasa kutokana na mchango wake ndani ya Liverpool haswa katika msimu wa 2017/18.

Nyota huyo Mmisiri ameweza kumaliza msimu akiwa mfungaji bora na akifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu nchini England.

No comments:

Post a Comment