MBAO FC YAINGIA KATIKA VITA NA YANGA KUMUWANIA MAVUGO - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 17 June 2018

MBAO FC YAINGIA KATIKA VITA NA YANGA KUMUWANIA MAVUGO


Uongozi wa Mbao FC, umesema ukipata tu fedha basi usajili wao wa kwanza ni kumvuta straika wa zamani wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Solly Njashi ameeleza kuwa wameamua kusaka fedha kwa ajili ya kuziba pengo la aliyekuwa mshambuliaji wao, Habib Kyombo.

Njashi anaamini kama endapo watapata fedha hizo wataweza kumshawishi Mavugo aweze kutua jijini Mwanza tayari kumalizana naye.

“Unajua kwa sasa hatuna mshambuliaji baada ya kuondoka kwa Habib Kyombo aliyetimkia Singida United, lakini tunaamini kama tukipata fedha ndani ya wakati hakika Mavugo atatua Mbao FC" alisema.

Kyombo alisajiliwa na Singida United siku kadhaa zilizopita na kusaini mkataba wa mika amitatu utakamfanya awe na timu hiyo mpaka mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment