MATUMAINI YA AFRIKA KOMBE LA DUNIA, SENEGAL YASUBIRIWA KWA HAMU LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 19 June 2018

MATUMAINI YA AFRIKA KOMBE LA DUNIA, SENEGAL YASUBIRIWA KWA HAMU LEO

Ukisema matumaini ya Waafrika kwa wawakilishi wao watano wa Kombe la Dunia huko Urusi yamekuwa finyu, hautakuwa umekosea.

Tunisia imekuwa timu ya nne ya Afrika kupoteza mechi mechi ya kwanza na kesho ni zamu wa Senegal. Hata hivyo, Tunisia pia imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kufunga bao katika Kombe la Dunia 2018.

Sasa timu zote nne za Afrika zimecheza mechi ya kwanza na kupoteza baada ya mechi ya jana ya Tunisia ambayo ilifungwa na England, Harry Kane akifunga bao katika dakika ya 90.

Kabla ya Tunisia, timu tatu za Afrika zilishacheza na kupoteza na hakuna iliyofunga bao. Timu ya 5 ya Afrika ni Senegal, itacheza kesho dhidi ya Poland. Kumbuka hakuna iliyoshinda wala kupata sare katika mechi zote za kwanza.

Matumaini ya kuwa Senegal ni timu ya mwisho ya Afrika inayocheza leo kama kweli itaweza kuwabeba Waafrika na kuibua matumaini kama kweli kuna timu ya Afrika inaweza kusonga mbele.


MATOKEO:
Misri 0-1 Uruguay
Morocco 0-1 Iran
Croatia 2-0 Nigeria
England 2-1 Tunisia

No comments:

Post a Comment