MARTIAL KUONDOKA MAN UNITED - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 14 June 2018

MARTIAL KUONDOKA MAN UNITED


Manchester United ya Uingereza imeshituliwa na habari kwamba mchezaji wake, Anthony Martial, anataka kuondoka.

Taarifa zilizopatikana kwenye klabu hiyo kupitia kwa Philippe Lamboley, ambaye ni mwakilishi wa Martial, zinasema juhudi za kumpatia mkataba mpya mchezaji huyo zimekuwa zikisuasua na hazieleweki vyema kwa muda wa miezi kadhaa sasa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye ameachwa katika timu ya taifa ya Ufaransa kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazofanyika Urusi, amekuwa na uhusiano mbaya na kocha Jose Mourinho kutokana na kiwango chake.

Mourinho alisema wazi kwamba uchezaji wake haumridhishi, hii ni baada ya timu hiyo kushindwa na Brighton mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment