MANENO YA BATSHUAYI BAADA YA KUTIKISA KAMBA ZA WATUNISIA LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

MANENO YA BATSHUAYI BAADA YA KUTIKISA KAMBA ZA WATUNISIA LEO


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Michy Batshuayi ameelezea furaha yake kufuatia kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia Urusi.

Batshuayi amefunga goli hilo mnamo dakika ya 90 wakati wakicheza dhidi ya Tunisia likiwa la kwanza kwake katika mashindano hayo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Batshuayi ameandika kuwa hatimaye ndoto yake imetimia kutokana na ushindi huo huku akisema goli halipi nafasi bali ushindi.Mabao mengine katika mchezo yamewekwa kimiani na Romelu Lukaku pamoja na Eden Hazard ambao wamefunga mawili kwa kila mmoja.

No comments:

Post a Comment