Mambo Hadharani Kuhusu Kitenge Kumuoa Zari Huu hapa Ukweli Wote - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 22 June 2018

Mambo Hadharani Kuhusu Kitenge Kumuoa Zari Huu hapa Ukweli Wote

 Kama ulisikiasikia minong’ono na kuona picha kwenye mitandao ya kijamii bila kujua ukweli wa ishu ya mtangazaji Maulid Kitenge kutinga Sauz, nyumbani kwa mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kudaiwa kutaka kumuoa, basi Amani limezungumza na Kitenge ‘live’, ameanika ukweli wa mambo ulivyo.

ISHU ILIANZA HIVI

Picha na video zinazomuonesha Kitenge akiwa nyumbani kwa Zari, zilisambaa usiku wa Jumapili iliyopita kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram na kuzua gumzo kwa wafuasi mbalimbali wa mitandao ya kijamii.

VIDEO ZENYEWE

Kwenye video hizo, Kitenge alionekana akiwa na watoto wa Zari akichezacheza nao huku Zari akiwa bize jikoni kuandaa msosi. Kwenye baadhi ya vipande vya video hizo, mtangazaji huyo wa EFM amesikika akimsifia Zari kuwa ni msafi na anajua kupika.

AGUSIA SUALA LA POSA

Katika vipande vingine vilivyopo mitandaoni, Kitenge alisikika akiwauliza mashabiki wake kama mrembo huyo wa Kiganda anafaa kuolewa au la.

“Nilete posa au nisilete?” alisikika Kitenge huku wafuasi wake mtandaoni wakimpa maoni tofautitofauti.

Kuna ambao walimwambia afanye kweli amuoe, kuna wengine wakamtaka amuache maana ataingia kwenye bifu zito na Diamond ambaye yupo kwenye harakati za mwishomwisho kurejesha penzi lake lililokuwa limevunjika.


KITENGE ASAKWA

Mara baada ya kukusanya maoni mbalimbali mitandaoni, Amani liliamua kumvutia waya Kitenge moja kwa moja akiwa Sauz wanaporusha matangazo ya Kiswahili ya Kombe la Dunia.

Hata hivyo, jitihada za kumpata Kitenge zilifanyika kwa siku nzima ya Jumatatu na kufanikiwa kumpata usiku wa saa nne kutokana na ubize wa kazi zake nchini Sauz.

TUJIUNGE NA KITENGE

Amani: Kaka vipi, tunataka kufahamu kuhusu picha zako na Zari zilizosambaa mitandaoni, tunaweza kujua mlikutana vipi na ‘mlispendi’ muda gani nyumbani kwake?

Kitenge: Alinialika kwake kwa lunch tu kama rafiki yake.

Amani: Rafiki yako sawa, mlikutana wapi hadi mkafikia hatua ya kwenda nyumbani kwake?

Kitenge: Kwanza tulikutana alipokuja hoteli tuliyofikia (Sauz) alikuwa na kikao na watu baadaye tukaonana hapo so kutokea hapo akanialika lunch kwake.

Amani: Oooh mbali na kupika vizuri kama tulivyosikia ukimsifia kwenye mitandao, Zari ni mwanamke wa aina gani anapokuwa nyumbani kwa jinsi ulivyomuona?

Kitenge: Ni mwanamke anayependa usafi na ni mwanamke ambaye akiwa nyumbani anakuwa mama kweli kwa kuwaangalia watoto, kuwajali pia wageni wake.

Amani: Sasa pale nyumbani kwake mbali na kula, mlifanya nini cha ziada?

Kitenge: Kanizungusha kuiona nyumba yake na anavyoishi, kwa kweli

ni mwanamke wa aina yake.

Amani: Lakini, zile video hazikuleta shida kwa mkeo Bongo alipoona unamsifia Zari kuwa anajua kupika na kuuliza kuwa upeleke posa?

Kitenge: Miye Muislamu hata hivyo na yeye Muislamu hajaolewa!

Amani: Kwa hiyo mkeo Bongo hakukunja hata mdomo?

Kitenge: Video hazikuleta shida.

Amani: Huku nchini Wabongo wamelipuka vibaya wanataka kusikia kauli yako upo ‘serious’ kweli unaweza kumng’oa Zari? Wanasema si unajua Diamond bado anataka kurudisha majeshi?

Kitenge: Si wameachana? Maana kaniambia anaishi mwenyewe na analea watoto.

Amani: Duuh sasa umemkaribisha na yeye huku? Lakini si anatambua na wewe una mke huku? (Kitenge ana wake wawili).

Kitenge: Hehe nimemkaribisha na tumekubaliana aje Agosti Dar.

Amani: Unataka kuniambia kwamba kama ataridhia unaweza kumuoa? Huoni kama italeta bifu kali kwa Diamond akija huku kwa ajili yako?

Kitenge: Hayo tutayazungumza yote!

Amani: Ok kaka nashukuru, nikutakie usiku mwema na kazi njema.

Kitenge: Ahsante usiku mwema.

UMEMUELEWA KITENGE?

Kutokana na mahojiano hayo ni dhahiri kwamba Kitenge anaweza kuingiza majeshi kwa Zari endapo watakubaliana kwa sababu amesema dini yake inamruhusu kuoa wake zaidi ya mmoja.

Na kwa vile amesema amemualika Agosti mwaka huu, tusikilizie na lolote linaweza kutokea!

ZARI VIPI?

Jitihada za kumpata Zari ili kuweza kusikia kauli yake kuhusu Kitenge hazikuzaa matunda kufuatia kuwepo na ugumu wa mawasiliano yake.

TUJIKUMBUSHE

Zari alitangaza kumwaga Diamond aliyezaa naye watoto wawili Februari 14, mwaka huu kwa kudai staa huyo wa Bongo Fleva amekuwa akimsaliti mara kwa mara.

Hata hivyo, hivi karibuni kwa nyakati tofauti Diamond na meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ wamefika Sauz kwa ajili ya kusaka suluhu ya uhusiano huo ambapo taarifa za awali zilieleza kwamba mazungumzo yao yalikuwa yanakwenda vizuri.
Chanzo: Global Publishers

No comments:

Post a Comment