Mama Atiwa Mbaroni Kwa Kumtupa Mtoto Wake Chooni - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 26 June 2018

Mama Atiwa Mbaroni Kwa Kumtupa Mtoto Wake ChooniRhobina Andrew (40) mkazi wa Kitongoji cha Nyatiti kijiji cha Buriba, kata ya Sirari wilayani hapa mkoani Mara, anashikiliwa na polisi akidaiwa kujifungua na kutupa kichanga kwenye choo cha shimo.


Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe, amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.


Amesema jeshi hilo lilimkamata Rhobina jana Juni 25 baada ya kupewa taarifa na wananchi ambako alifikishwa kituo cha polisi Sirari.


Mwenyekiti wa Kitongoji cha Buriba, Alex Chacha alisema alipigiwa simu Juni 25 na mkazi wa kitongoji hicho na kuelezwa kuwa mtoto huyo ameokotwa kwenye tundu la choo akiwa hai.


“Tulfanikiwa kubomoa choo na kutoa mtoto akiwa hai, tukamwosha kwa kuwa hakuwa amefunikwa chochote mwilini lakini wakati tunampeleka kituo cha afya akafariki dunia," amesema Chacha.

No comments:

Post a Comment