Mahakama ya Juu Zaidi Marekani Yaidhinisha Marufuku ya Usafiri ya Trump kwa Nchi za Kiislamu - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 26 June 2018

Mahakama ya Juu Zaidi Marekani Yaidhinisha Marufuku ya Usafiri ya Trump kwa Nchi za Kiislamu

Mahakama ya juu zaidi Marekani imeidhinisha marufuku ya usafiri ya utawala wa rais Trump inayowalenga raia kutoka nchi kadhaa za Kiislamu.

Mahakama za chini zilitaja marufuku hiyo kwenda kinyume na katiba, lakini mahakama hiyo ya juu zaidi imepindua uamuzi huu kwa ridhaa ya baadhi ya majaji katika tangazo lililotolewa Jumanne.

Marufuku hiyo inawazuia raia kutoka mataifa ya Somalia, Libya, Iran, Syria na Yemen kuingia Marekani

Kumekuwa na shutuma kali kutoka kwa wakimbizi na mashirika ya kutetea haki za binaadamu dhidi ya marufuku hiyo.

No comments:

Post a Comment