Magari ya Polisi, Ambulance na JWTZ Yanazovunja Sheria Yapewa Onyo Kali - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 14 June 2018

Magari ya Polisi, Ambulance na JWTZ Yanazovunja Sheria Yapewa Onyo Kali

Kamanda wa Jeshi la polisi Kanda Maalum, Lazaro Mabosasa limepiga marufuku magari ya serikali, magari ya vyombo vya ulinzi na usalama na yale ya wagonjwa kupita kwenye barabara zisizoruhusiwa kwa kuwa sio matumizi salama.

Mabosasa ametoa marufuku hiyo ikiwa ni siku tatu baada ya gari la wagonjwa la Chuo Kikuu cha DSM kuligonga lori na kusababisha vifo vya watu wa wanne wakiwamo wanafunzi wawili wa chuo hicho.

“Barabara imetengwa kwa ajili ya magari yaendayo kasi matokeo yake wanaleta vurugu na wengine kusababisha ajali” amesema Mambosasa.

No comments:

Post a Comment