Maalim Seif aanza ziara, wananchi watakiwa kuonyesha ushirikiano - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 9 June 2018

Maalim Seif aanza ziara, wananchi watakiwa kuonyesha ushirikiano


Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameanza ziara ya siku mbili kisiwani Pemba leo.

Mkurugenzi wa habari wa chama hicho upande wa Maalim Seif, Salim Abdalla Bimani amesema leo kuwa ziara hiyo ni ya kawaida kwa kiongozi huyo kila ifikapo mwezi wa Ramadhan.

Amesema ziara hiyo haihusiani na harakati za chama bali ni kuwajulia hali wagonjwa na kuwapa pole wafiwa kama ilivyo kawaida yake.

Katika ziara hiyo ya siku mbili anatarajiwa kutembelea mikoa yote miwili ya kisiwa hicho na kisha kurudi kisiwani Unguja kuendelea na ziara kama hiyo katika maeneo mbali mbali.

Bimani amewataka wananchi wa kisiwani hicho cha Pemba kutoa ushirikiano wao wa kina kwa kiongozi huyo wa chama chao.

No comments:

Post a Comment