LIGI KUU ENGLAND IMEFUNIKA ZAIDI KOMBE LA DUNIA RUSSIA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 10 June 2018

LIGI KUU ENGLAND IMEFUNIKA ZAIDI KOMBE LA DUNIA RUSSIA


NA SALEH ALLY
UNAWEZA ukashangazwa na Ligi Kuu England kwamba pamoja na kupewa sifa ya kuwa ligi bora, lakini imekuwa haina timu zinazobfanya vizuri zaidi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu uliomalizika hivi karibuni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, umekuwa na nafuu kubwa kwa England baada ya Liverpool kuingia fainali.

Lakini utaona kabla ya hapo kulikuwa na ugumu kwa England kupata nafasi hiyo na timu za Hispania zikatawala kwa kiasi kikubwa.

Hiyo haikuisaidia kuiondolea England ubora wake wa kuwa ligi ngumu, yenye ushindani wa kweli unaohitaji nguvu na ujuzi wa juu ili mchezaji kuwa mshindani sahihi katika LIgi Kuu England maarufu kama EPL.

Sasa akili ya wapenda soka inaelekezwa Kombe la Dunia ambako wachezaji wote nyota wa soka au kwa asilimia 78 watakuwa Russia katika michuano hiyo.

Mechi 64 zitachezwa na hapa nyumbani zitaonekana katika king’amuzi cha StarTimes ambacho kitarusha kwa lugha ya Kiswahili.

Macho na masikio yatakuwa Russia ambako kila timu iko tayari kwa michuano hiyo na kinachovutia kingine kutoka England ni kwamba, ndiyo ligi inayoongoza kutoa wachezaji wengi zaidi katika Kombe la Dunia.

Yaani kama utahesabu wachezaji kutoka katika kila timu, England au Ligi Kuu England ndiyo iliyotoa wachezaji wengi zaidi.

Kwa jumla, EPL imetoa wachezaji wengi zaidi kwa kuwa ina 100 kutoka katika timu mbalimbali na hata zile ambazo haikutarajiwa kuonekana ina wachezaji.

Maana yake, timu zinazoshiriki Kombe la Dunia zimechukua wachezaji wengi zaidi kutoka katika EPL, hii inaonyesha ubora wake umewavuta makocha wengi zaidi kuhakikisha wana watu kutoka katika ligi hiyo.

Hii inazidi kuipaisha England na kuonekana kweli ina ligi bora au ligi ngumu ambayo inastahili kupendwa zaidi duniani kwa kuwa kimahesabu, Kombe la Dunia ni sawa na bora wa juu zaidi wanaocheza michuano mikubwa zaidi ya soka duniani.

Kwa wachezaji, Kombe la Dunia kama mshiriki ni heshima kubwa sana. Maana kuna wachezaji wengi bora hawakuwahi kucheza michuano hiyo mikubwa zaidi.

Unaweza ukashangazwa zaidi na England kwa kuwa ungeweza kutegemea ingekuwa na wachezaji wengi zaidi katika timu kama Australia, lakini inashangaza kuona England inaongoza kwa kuwa na wachezaji wengi katika timu kama Argentina.

Ndani ya Argentina ina wachezaji watano sawa na Italia. Kiutamaduni, Argentina inacheza zaidi kwa mfumo kutoka Hispania au Italia. Lakini mwisho unaona Hispania kuna wachezaji watatu tu wanaotokea katika La Liga wakiongozwa na nahodha Lionel Messi.

England ina wachezaji saba kutoka Australia na inaongoza kuliko nchi nyingine, zinazofuatia zina wachezaji wawili tu kila moja.

Hata Misri, England inaongoza maana katika kikosi hicho cha mafarao kuna wachezaji saba akiwemo Mo Salah wanaotokea England, kumbuka inaweza kuwa EPL au ligi daraja la kwanza lakini hii bado inabaki kuwa sifa ya soka la England kuwa linaaminika zaidi.

Makocha wengi zaidi kuchagua wachezaji wengi zaidi kutoka EPL au England inaonyesha soka la nchi hiyo linaaminika zaidi.

Unaona England imesambaza wachezaji katika mabara yote, kuanzia Ulaya, Afrika, Asia, Amerika Kusini, Australia na kadhalika na mwisho kufikisha idadi ya wachezaji 100.

Wanaowafuatia ni Hispania na utaona wako mbali, maana wao wana wachezaji 64 na Italia ni ya tatu ikiwa na wachezaji 58 wanaocheza nchini humo.

Ujerumani ambayo ungeweza kuipa nafasi kubwa kupitia Bundesliga, yenyewe imepeleka wachezaji 52, Ufaransa ni 39 na Uturuki imejitutumua kuwa na wachezaji 22 ikifuatiwa na Marekani.

Hakuna ubishi kwamba makocha huangalia sehemu yenye ubora kwa ajili ya kujenga sehemu bora ya kikosi.

Inaonekana Kombe la Dunia nchini Russia, kipimo cha ubora cha makocha wengi, kimeangukia England na hii inathibitisha kwamba ubora katika nchi hiyo, uko juu sana.

Maana yake, kama utafanikiwa kuona mechi za Kombe la Dunia, kuna nafasi kubwa ya kuwaona wachezaji 100 kutoka EPL au England wakishiriki michuano hiyo.

Maana yake, pamoja na yote, katika michuano hiyo, ladha ya England itaendelea kuonekana wakati wa mwezi mmoja wa michuano hiyo.


VIKOSI NA WACHEZAJI KUTOKA KATIKA LIGI MBALIMBALI:

Argentina (22): England (5), Italy (5), Spain (3), France (2), Germany (2), Mexico (1), Netherlands (1), Portugal (1), China (1), South Korea (1)
Australia (17): England (7), Japan (2), Switzerland (2), Scotland (2), Netherlands (1), Saudi Arabia (1), Turkey (1), Belgium (1)
Belgium (22): England (11), Germany (3), Spain (2), France (2), China (2), Italy (1), Scotland (1)
Brazil (20): England (6), Spain (5), Italy (3), France (3), Ukraine (2), China (1)
Colombia (20) : Spain (6), Argentina (3), England (3), Mexico (2), Italy (2), Netherlands (1), France (1), Germany (1), Brazil (1)
Costa Rica (17) : USA (5), Spain (4), Italy (1), Portugal (1), Canada (1), England (1), Switzerland (1), Scotland (1), Colombia (1), Sweden (1)
Croatia (21): Italy (6), Spain (4), Germany (4), France (1), England (1), Turkey (1), Belgium (1), Ukraine (1), Russia (1), Austria (1)
Denmark (20) : England (7), Spain (3), Germany (3), Netherlands (3), Italy (2), France (2)
England (0)
Egypt (16): England (7), Saudi Arabia (4), USA (1), Finland (1), Turkey (1), Greece (1)
France (14): Spain (6), England (5), Germany (2), Italy (1)
Germany (8): England (3), Spain (2), France (2), Italy (1)
Iceland (22): England (5), Denmark (3), Russia (3), Germany (2), Netherlands (1), Italy (1), Scotland (1), Turkey (1), Belgium (1), Sweden (1), Norway (1), Bulgaria (1), Wales (1)
Iran (14): Russia (3), Greece (3), Netherlands (2), Qatar (2), Portugal (1), England (1), Belgium (1), Sweden (1)
Japan (15): Germany (7)England (2), Spain (2), France (2), Mexico (1), Turkey (1)
Mexico (12): Portugal (4), Spain (3), Germany (2), Netherlands (1), England (1), Belgium (1)
Morocco (21): Spain (6), Turkey (4), Netherlands (3), France (2), Germany (2), Italy (1), England (1), Belgium (1), UAE (1)
Nigeria (21): England (4), Turkey (4), Spain (2), Russia (2), Italy (2), China (2), France (1), Netherlands (1), Germany (1), Belgium (1), Israel (1)

Yoshimar Yotun, left. (AP Photo/John Raoux)
Panama (21): USA (6), Guatamela (2), Chile (2), Peru (2), Spain (1), Mexico (1), Belgium (1), Colombia (1), Costa Rica (1), Romania (1), Slovakia (1), Honduras (1)
Peru (15): Mexico (7), Brazil (3), Netherlands (1), Portugal (1), Colombia (1), Russia (1), Denmark (1)
Poland (19):  Italy (7), England (4), Germany (3), France (1), Belgium (1), Russia (1), Bulgaria (1), Wales (1)
Portugal (17): England (4), Turkey (3), Spain (2), Italy (2), France (2), China (1), Germany (1), Scotland (1), Russia (1)
Russia (2): Spain (1), Belgium (1)
Saudi Arabia (3): Spain (3)
Senegal (23): France (7), England (7), Italy (3), Turkey (2), Belgium (2) Germany (1), Guinea (1)
Serbia (20):  Italy (4), England (4), Germany (3), Spain (2), Portugal (1), Turkey (1), Belgium (1), Russia (1), Wales (1), Greece (1), Israel (1)
South Korea (10): Japan (5), Italy (1), England (1), Germany (1), Austria (1), Wales (1)
Spain (6): England (4), Italy (1), Germany (1)
Sweden (21): Italy (4), France (3), England (3), Germany (3), Wales (2), Spain (1), Scotland (1), Belgium (1), Russia (1), Denmark (1), UAE (1)
Switzerland (22): Germany (10), Italy (5), England (2), Spain (1), Portugal (1), France (1), Turkey (1), Croatia (1)
Tunisia (17): France (7), Saudi Arabia (5), Egypt (2), England (1), Turkey (1), Belgium (1)
Uruguay (21): Spain (5), Italy (5), Argentina (3), Mexico (2), Portugal (2), Belgium (2), France (1), Turkey (1)

(Photo by Denis Doyle/Getty Images)

IDADI YA WACHEZAJI WA LIGI MAARUFU KATIKA KOMBE LA DUNIA 
England — 100
Hispania — 64
Italia — 58
Ujerumani — 52
Ufaransa — 39
Uturuki — 22
Marekani — 18
Ubelgiji — 17
Uholanzi — 15
Mexico — 14
Ureno — 10
Saudi Arabia — 10
China — 7
Japan — 7
Scotland — 7
Argentina — 6
Wales — 6
Denmark — 5
Ugiriki — 5
Brazil — 4
Colombia — 3
Sweden — 3
Switzerland — 3
Ukraine — 3
Chile — 2
MisriSo — 2
Guatemala — 2
Israel — 2
Peru — 2
Qatar — 2
UAE — 2
Austria – 1
Bulgaria — 1
Canada — 1
Costa Rica — 1
Croatia — 1
Finland — 1
Guinea — 1
Honduras — 1
Norway — 1
Romania — 1
Slovakia — 1
South Korea — 1
SOURCE: SPOTI XTRA

No comments:

Post a Comment