KOCHA MPYA REAL MADRID HUYU HAPA, AKIMALIZA KAZI URUSI NDIYO ATAANZA KAZI - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 12 June 2018

KOCHA MPYA REAL MADRID HUYU HAPA, AKIMALIZA KAZI URUSI NDIYO ATAANZA KAZI

 Kocha Julen Lopetegui ametangazwa kuchukua mikoba ya Kocha Zinedine Zidane aliyeamua kuachia ngazi.

Lopetegui mwenye umri wa miaka 51 kwa sasa anainoa timu ya taifa ya Hispania inayoshiriki Kombe la Dunia.

Kocha huyo kijana ataanza kazi mara moja baada ya michuano ya Kombe la Dunia.

Baada ya kujiuzulu kwa Zidane Mei 31, mwaka huu kulikuwa na majina ya makocha wengi kama Antonio Conte wa Chelsea, Jurgen Klopp wa Liverpool na Mauricio Pochettino wa Tottenham alipewa nafasi kubwa.

No comments:

Post a Comment