KOCHA JULIO ASEMA ALIKIBA ANASTAHILI KUCHEZA SOKA ULAYA, MENGI AMEFUNGUKA HAPA - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 11 June 2018

KOCHA JULIO ASEMA ALIKIBA ANASTAHILI KUCHEZA SOKA ULAYA, MENGI AMEFUNGUKA HAPA


Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameweka wazi kuwa msa­nii wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’ ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza Ligi Kuu Bara, na kama aki­andaliwa vizuri anaweza kucheza hata Ulaya.

Kwa mjubu wa gazeti la Championi, Julio ameyasema hayo akiwa kocha wa Team Sa­matta mara baada ya kum­alizika kwa mchezo maalum wa kuchangia elimu ulio­andaliwa na msanii huyo akishirikiana na Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa katika Klabu ya Genk nchini Ubelgiji.

Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar, Team Samatta iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Team Kiba.

Akizungumza na Champi­oni Jumatatu, Julio alisema msanii huyo ni mchezaji mzuri na amekuwa akim­wambia kuwa yupo tayari kumsajili achezee katika timu yake kutokana na uwezo mkubwa alionao na kama akiwekwa vizuri ana uwezo wa kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

“Alikiba ni mchezaji mzuri sana, mimi binafsi huwa namwambia ‘nataka nikusa­jili’, kama hawezi kuja kule mkoani lakini tukija hapa Dar aje acheze, ana uwezo mkubwa­ sana kuliko wachezaji wengi wa Simba na Yanga ambao wanalipwa mishahara ya bure.

“Isipokuwa tu nchi yetu haitaki kujua watu wenye uwezo, tunafua­ta majina na labda wana sababu zao, ndiyo hivyo lakini Kiba kama anatengenezwa hakuna ambaye anaweza kusema kuwa Kiba siyo mchezaji na kwa uwezo wake kama anacheza basi hapa ata­cheza ligi hii, mwaka wake mmoja tu anakwenda kucheza soka la kulipwa,” alisema Julio.

No comments:

Post a Comment