KISA YANGA, WAWA AANZA MIKWARA - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 13 June 2018

KISA YANGA, WAWA AANZA MIKWARA


Beki wa kimataifa raia wa Ivory Coast, Pascal Serge Wawa, amesema kuwa, kwa sasa yupo kwenye maandalizi kabambe ya kutua kwenye kikosi cha Yanga ambapo muda wowote kuanzia sasa anaweza kuwa mchezaji wa timu hiyo.

Wawa ambaye amekuwa akiwindwa kwa hali na mali na Yanga, amesema wala hawezi kukataa kujiunga na timu hiyo ndiyo maana ameanza mazoezi mapema ili akijiunga na timu hiyo awe fiti kupambana.

Wawa ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, aliwahi kuitumikia Azam FC kabla ya mwishoni mwa mwaka 2016 kuhamia El-Merreikh ya Su­dan aliposaini mkataba wa miaka miwili ambao tayari umemalizika.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Wawa mwenye mwili mkubwa amesema amekuwa akifanya mazoezi binafsi kila siku yakiwemo ya uwanjani na kukimbia barabarani ili akija Yanga awe fiti asilimia 100.

“Kila Jumamosi na Jumapili huwa nakimbia barabarani kujiweka fiti na huwa siangalii nimekimbia umbali wa kilomita ngapi, bali unakuwa umbali mrefu sana. Siku zinazobakia huwa nafanya mazoezi ya uwan­jani.

“Nafanya hivi ili niwe fiti zaidi ili nikitua Yanga niwe tayari kwa kuitu­mikia timu, kwa kuwa wenyewe wameonyesha nia ya kunihitaji, siwezi kukataa ofa yao, nitakuja tu kuichezea kwa msimu ujao.

“Nataka nikija niwe fiti kuingia uwanjani na siyo kuanza tena kufanya maandalizi kwa kuwa najiamini kuwa naweza kazi,” alisema Wawa. 

No comments:

Post a Comment