KIKOSI CHA SIMBA CHAREJEA USIKU NCHINI, SABABU YA KUWAHI NI HII - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 11 June 2018

KIKOSI CHA SIMBA CHAREJEA USIKU NCHINI, SABABU YA KUWAHI NI HII


Kikosi cha Simba kimerejea nchini usiku wa jana kikitoea, Nakuru, Kenya ambako kilienda kushiriki mashindano ya SportPesa Super CUP.

Kikosi hicho kimerudi ikiwa ni baada ya kupoteza mchezo wa fainali kw ajumla ya mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Afraha.

Kwa mujibu wa Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema wamewahi kurejea kwa ajili ya halfa maalum ya uhawajwi wa tuzo za wachezaji wao unaofanyika leo kwenye Hotel ya Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zinazojulikana kama Mo Simba Awards, zitatolewa kwa viongozi, wachezaji, tawi na shabiki bora kwa msimu wa 2017/18.

Kwa mujibu wa mwanzilishi wa tuzo hizo, Mohammed Dewji 'Mo. amesema lengo kubwa la kuazishwa kwa tuzo hizo ni kutambua mchango wa walofanikisha kupata mafanikio makubwa ndani ya klabu ikiwemo ubingwa wa ligi kwa msimu uliomalizika.

No comments:

Post a Comment